12 May 2016 1 Min Read
Polisi Wamtaka Wetangula Kutoa Taarifa Kuhusu Mauaji Ya Jacob Juma
by Brian Ndungu Habari
Polisi wanamtaka seneta wa Bungoma Moses Wetang’ula kuwapa taarifa kuhusu mauaji ya mfanyibiashara Jacob Juma ili kusaidia katika uchunguzi.
Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet pia ameomba yeyote aliye na taarifa kuhusu mauaji hayo, kuiwasilisha katika kituo cha polisi kilicho karibu.
Wetang’ula alikua amesema atawataja waliohusika na mauaji ya Jacob Juma wakati wa mazishi yake siku ya jumamosi.
Huku haya yakijiri, leo Umma utaruhusiwa kuutazama mwili wa mfanyibiashara huyo katika bustani ya uhuru. Shughuli nyingine kama hiyo pia itaandaliwa mjini Kakamega siku ya jumamosi kabla ya mazishi yake.