rsz_fa_cup_2

Kwa kila shabiki wa mpira wa miguu almaarufu kabumbu, ndoto kuu ni aidha kuhudhuria mechi moja au kadhaa ambayo timu aipendayo inacheza au pia kupata fursa ya kukutana na kutangamana na wachezaji wa sasa au wa kale wa timu aishabikiayo.

Basi ndoto hii iligeuka kuwa hali ilivyo kwa mtangazaji maarufu wa Jacob Ghost Mulee, shabiki sugu wa Manchester United, ambaye alipata fursa ya kuburudika na kombe la FA ambalo timu yake ya Manchester ilitwaa msimu uliopita na kusawazisha rekodi ya Arsenal kama vilabu vilivyotwaa mataji mengi (12) ya FA.

Ghost Mulee ambaye alishiriki kama mchezaji wa timu ya Tusker na pia Harambee Stars kabla ya kuwa kocha wa timu ya taifa, Harambee Stars mara mbili, bado yuko katika ulingo wa kandanda huku akiwa mkuza vipaji katika chuo cha soka cha Liberty ambacho kimekuza vipaji kama Michael Olunga.

Hapo jana Mulee alipata fursa ya kuzuru na kombe hilo lenye umaarufu zaidi Uingereza katika maeneo tofuati humu nchini, mojawapo ikiwa chuo cha Liberty huku akiandamana naye gwiji wa soka Uingereza, David James ambaye kama mwenzake Ghost Mulee, alicheza katika safu ya ulinzi kama mlinda lango.

Tazama picha zifuatazo.

View Comments