21 October 2016 1 Min Read
Msilete siasa katika mazishi ya mtoto wangu aomba mbunge Olago Aluoch
by Maureen Waruinge Habari
Mbunge wa Kisumu Magharibi Olago Aluoch ametoa wito kwa wanasiasa watakaohudhuria hafla ya mazishi ya mtoto wake kuepukana na siasa wakati wa hafla hiyo hiyo kesho.
Kando na viongozi wa kisiasa mbunge huyo vile vile amewataka wakaazi watakaohudhuria kutoshirikisha hafla hiyo ya mazishi ya binti yake na siasa.
Kulingana na Olago, kama familia wangependa kutoa heshima zao za mwisho kwa mtoto wao Joyce Aluoch, aliyeaga dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani kwenye.
Hafla hiyo inatazamiwa kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali.
Ibada ya maombi itaandaliwa kwenye uwanja wa maonyesho ya Klimo mjini Kisumu.