Mwalimu mmoja katika shule ya msingi ya Nyikendo kwenye kaunti ya Migori anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa miaka kumi na sita wa darasa la nane na kumpachika mimba.

Kulingana na babake mwanafunzi huyo Peterlis Omutu, mwalimu huyo anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo wa darasa la nane kuanzia mwishoni mwa mwaka jana.

Mzazi huyo anataka haki kutendeka na mwalimu huyo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kumpachika mimba na kumbaka kinyume cha sheria.

Mwanafunzi huyo pia alikiri kuwa mwalimu huyo amekuwa akimchukua kutoka kwao nyumbani na kumpeleka mjini Migori katika vyumba vya burudani ambako wawili hao wamekuwa wakifanya mapenzi.

Juhudi za kutafuta majibu kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo hazikufua dafu baada yake kuwa kwenye mkutano na wasimamizi wa shule hiyo na kusema kuwa bado anafanya uchunguzi kuhusu kisa hicho na kuwa hangezungumzia swala hilo hadi uchunguzi huo kukamilika.

View Comments