mhudumu
Mhudumu wa bodaboda kutoka Kakamega aliyesemekana kumnunua mke wa mwenzake kwa shilingi mia tano mjini kakamega, sasa amemrejesha mke huyo kwa mwenyewe.
Mhudumu huyo amesema mwenzake amelalama upweke na kibaridi na ikamlazimu kumwonea huruma.
Mhudumu mwenzake wa bodaboda alimuuzia mkewe kwa shilingi mia tano kujipatia posho la kusherehekea krismasi na chupa ya soda.
Inasemekana mhudumu huyo mwenye umri wa miaka thelathini na miwili anayejulikana kwa jina la utani 'Tusker' alipatiana mkewe kama dhamana ya fedha alizozihitaji kwani mapato yake hayangemruhusu kupata hela hizo.
Marafiki wake walisema kuwa mnunuzi aliyetambulika kama 'Small' alikuwa anammezea mate mkewe 'Tusker' kwa mda mrefu lakini hangemtongoza, kwa ajili ya urafiki wa wawili hao.

Mwanamke huyo alidhibitisha kuwa bwanake alikubali mpangilio huyo na kuwa angelala kwa 'Small' kuanzia siku kuu ya Krismasi hadi tarehe moja Januari kwani hakuwa na fedha za kumtosheleza mahitaji yake kama mkewe.

Dunia imepasuka kweli.