Hivi majuzi Abraham Mureithi mwenye umri wa miaka 27, aliomba apatanishwe na mkewe Fridah 24, aliyeondoka nyumbani kwao mnamo Disemba 24 mwaka uliopita.

Akijieleza, bwana Abraham alisema kuwa mkewe alipata ujumbe kwa simu yake huku kutoka kwa mwanamke aliyekuwa akieleza jinsi alikuwa amemkosa kwa siku nyingi na isitoshe mwanamke huyo ni rafikiye Fridah.

"Sina uhusiano wowote na mwanadada huyo na nashuku nikama ilikuwa mpango wao wawili kuua ndoa yetu. Kuamka asubuhi iliyofuata nikaelekea kazini na niliporudi nikapata mke wangu na baba yake lakini hamna aliyetaka kuniskiza." Alisimulia Abraham akiongeza kuwa licha ya hayo bado anamshughulikia kwani wawili hao wana mtoto mmoja katika ndoa ya miaka mitatu.

Wakti Fridah alipopigiwa simu alifichua kuwa kando na kuwa na mipango ya kando, bwana Abraham alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe licha yake kuwa na shida za kimatibabu jambo lililomkasirisha.

"Mwanadada aliyemtumia ujumbe alibadilisha jina lake katika simu yake na kumbandika 'slim' ili nisijue, kufanya upelelezi kwa umakini kumbe ni rafiki yangu. Sioni kama nitaweza rudiana naye kwani huwa habadiliki." Alisimulia Fridah.

Mtu anaweza chunwa aingie kwa jirani? aliuliza Fridah akidhibitisha kuwa hakuchunwa ila alipigwa mara kwa mara.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be