mudavadi

Kiongozi wa chama cha Amani National Congress, Musalia Mudavadi alizuru studio za Radio Jambo siku ya Jumanne huku wenyeji wake wakiwa Gidi na Ghost.

Miongoni mwa yale alizungumzia mheshimiwa Mudavadi aliangazia muhula wa chama cha Jubilee serikalini ukiongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, muungano wa NASA ambao unawajumuisha viongozi kutoka vyama mbalimbali wakiwemo vinara wa CORD; Raila Odinga, Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka ambao wanawakilisha upinzani.

Huku akiwa mmoja wa waanzilishi wa muungano wa NASA, Mudavadi ana imani kuwa wote wakishikamana watang'oa serikali ya Jubilee mamlakani licha yao kutotaja nani atakayepeperusha bendera yao, wakti wa uchaguzi mkuu.

"Hapo jana katika mkutano wa NASA, mimi pamoja na waheshimiwa Raila, Kalonzo na Wetangula tulikutana na kujadiliana safari ambayo tunataka tuichukue tukikaribia uchaguzi na leo tuna mkutano na wanahabari ili tueleze wakenye ni lipi tulilojadiliana." Alisema Mudavadi.

"Kama NASA, tunataka tuwe na msingi mwema ambao utahakikisha sisi viongozi wa upinzani tunashirikiana kila mtu ni kiongozi wa chama tofauti lakini si sote ni jamii ya upinzani na tulipokutana lengo letu halikuwa kuzindua nani atakuwa mwakilishi katika uchaguzi mkuu ni lazima kwanza tuhakikishe kila cchama, kila mtu anajiskia sawa katika hema hii kubwa ya NASA." Aliongeza Mudavadi ambaye aliwahi kuwa naibu wa rais kuanzia tarehe 4 November 2002 hadi tarehe 3 January 2003, chini yake Rais Mstaafu Daniel Arap Moi.

Skiza mahojiano yafuatayo kupata uhondo kamili.

&feature=youtu.be