- steve
- patanisho 1

Mojawapo ya siku ambazo huwa zimengojewa sana kila mwaka ni; Siku ya kuzaliwa, siku krismasi, siku kuu ya pasaka na pia siku ya wapendanao, almaarufu 'Valentines' day' kwa kimombo.

Siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 14, mwezi wa Februari ambapo wapendanao hutumia fursa hiyo huonesha upendo kwa wake na bwana zao, huku wasiofanikiwa wakijaribu kutafuta wachumba siku iyo hiyo.

Siku hiyo wengi wa wapendanao huvalia nguo za rangi ya nyekundu kwani ndio rangi rasmi inayowakilisha upendo.

Basi leo ikiwa tarehe saba mwezi wa Februari, ni dhahiri kuwa siku ya wapendanao imekaribia na yaja kwa kasi mno kwani ni wiki moja tu.

Gidi alipokea ujumbe wa kuchesha kutoka kwa msikilizaji kuhusu wanaume na wanandoa ambao wamepanga kususia siku hiyo ya wapendanao huku wakianza mgomo kuanzia tarehe 12 hadi tarehe 15 siku moja baada ya siku kamili.

Huku Gidi akisoma ujumbe huo, mwenzake bwana Mulee aliangua kicheko na kuapa kuwa yumo tayari kuungana na wanaume hao kwani Njaanuari ilimkamua fedha nyingi na hana budi ila kugoma, bila kujali majuto kutoka kwa mkewe mpendwa.

"Utashiriki mgomo ama unaogopa mke kusikia?" Gidi alimuuliza bwana Ghost Mulee.

"Apana mimi pia niko kwa huo mgomo, nimeungana na wenzangu manake Januari imetumaliza halafu tena tarehe kumi na nne ituue bana?" Alijibu Mulee.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be