Baranaba 35, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Sarah mwenye umri wa miaka 30, ambaye walikosana miaka minne iliyopita. Licha ya miaka hiyo yote, Baranaba aliamua sasa ndio nafasi ya kipekee ya kumuomba msamaha.

Kulingana na bwana Baranaba, mkewe ambaye wamezaa pamoja watoto watatu, bado hajaolewa tangia wawachane miaka mitatu iliyopita na kila anapo muomba msamaha anakiri ampe nafasi ya kufikiria.

"Ilianza na haya maneno ya team mafisi ambapo kuna jamaa ambaye alikuwa akimnyemelea na baada ya mda mfupi yule jamaa akamnyakua na kumpa mimba. Walianza kukosana tu kwani hata walipokuwa pamoja walikuwa wanavurugana na hapo wakatengana. Watoto wetu ambao mie ndiye ninaishi nao huniuliza kila mara kuhusu mama yao. Saa hii ana mtoto na ule jamaa." alisimulia Baranaba.

"Sijui sana shetani aliyeingilia lakini kuna mambo fulani tulikosana ki ghafla, alianza kunitolea vitu kwa nyumba, kidogo nikapata TV hakuna, DVD haiko na anaenda nazo harudishi wala haniambii chanzo cha kuitoa. Tangu tuoane sikuwahi enda nje ya ndoa. Mwanaume anayedai alikuwa mpango wangu wa kando tulipatana naye baada ya visanga hivo vyote."

Alijieleza naye Sarah huku akidai atarudi tu mumewe akielekea kwao na kukutana na mamake.

Pata Uhondo kamili.

&feature=youtu.be