21 March 2017 1 Min Read
Madaktari wa Tanzania hawataki kuja Kenya
by Yusuf Juma Habari
Chama cha Madaktari nchini Tanzania kimepinga mpango wa kuwatuma madaktari 500 humu nchini wakisema Tanzania ina upungufu mkubwa wa madaktari.
Hii inafuatia makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Kenya mwishoni mwa wiki ambapo madaktari wapatao 500 watapata ajira nchini Kenya.
chama hicho pia kimeelezea hofu kuhusu usalama wa madaktari hao kwani kuna pingamizi kutoka kwa viongozi wa upinzani kuhusu mpango huo.