16649565_647102085477744_6951482243422551022_n

Janet 33, kadogo aomba apatanishwe na muwewe mwenye umri wa miaka 35 kwani amekaa miaka mitano nje ya ndoa tangu wakosane naye.

Wawili hao walijaliwa na watoto wawili wa kike.

"Nataka kurudiana naye kwa sababu ya vitu alinifanyia na yale alifanyia watoto wangu, sana sana mapenzi. Ilifanyika wakti mmoja nilipofanyiwa upasuaji na aliponifikisha nyumbani, akaniambia kuwa amemalizana nami na kuondoka bila hata kunipa sababu.

Nilimbembeleza turudiane lakini aliniarifu kuwa amepata madam mwingine msomi kumbe alikuwa dadake mdogo. Wawili hao walijaliwa mtoto mmoja lakini jamii ailiwatenganisha kwani nikama hakuwa na habari." Alieleza Janet akisema kuwa anataka sana warudiane na mumewe hata kama atarudi kama mjakazi wa watoto wake.

Alipopigiwa simu bwana Isaac alidai kuwa mkewe anafaa ampe nafasi kiasi ili afikirie maneno yale. "Sijatafuta mke au mambo ya dunia nimetafuta mungu pekee, wacha tu anipe mda mimi mwenyewe ndiye nitamtafuta kwani nimeng'ang'ana sana na watoto kuosha mkojo na kazi ya juakali na nashukuru mungu watoto wamekuwa wakubwa." Alisema Isaac.

Pata uhondo.