11 May 2017 1 Min Read
Tumia bidhaa za nyumbani kupata mkopo
by Yusuf Juma Habari
Sasa hauna sababu kama kijana kukosa pesa za kuanza kufanyia biashara.
Unaweza kutumia vifaa vya nyumbani, mifugo na hata mimea kama kinga ya kupewa mkopo na benki.
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini mswada unaowaruhusu watu kutumia vitu kama runinga, fanicha au hata gari kupewa mikopo.