Mwanadada kwa jina Jackie alituma ujumbe akiomba apatanishwe na aliyekuwa mumewe, Sebastian na mama mkwe kwani alikiri kuwa aliwakosea sana na baada ya hayo Sebastian akaamua kumuacha na kumuoa mwanamke mwingine.

Kulingana na bi Jackie, mama mkwe ndiye aliyeleta fitina kati ya wawili hao na kupelekea wawili hao kutengana.

Alipopigiwa simu, bwana Sebastian alieleza kuwa Jackie alikuwa mpenzi wake miaka ya jadi lakini sasa hivi ashafunga ndoa na mwanadada mwingine.

"Alikuwa mpenzi wangu sikuwa nimemuoa, lakini sasa yeye ni muhimu anene ukweli kwani ni jambo la busara. Kwanza nimefungulia redio ili mke wangu askize asije akaharibu ndoa. Kwanza aliwacha shule ili nimuoe na mimi nikamueleza kwanza asome kwani hamna tutakapopelekana naye." Alieleza Sebastian kabla ya kumpokeza mkewe Immaculate, simu.

"Tumeoana na mume wangu kwa takriban miaka mitatu sasa na tunapendana sana." Alisema Immaculate.

Jackie naye anasema kuwa alikuwa kwake mwaka uliopita mwezi wa tano na hakuwa ameoa na kwamba anashtuka kuwa eti wameoana kwa miaka mitatu.

"Gidi wanajaribu kudanganya kwani Immaculate amemleta juzi juzi tu kwani mimi niliishi na Sebastian kwa miaka miwili na mamake ndiye aliyekuwa ananiharakisha nimzalie mwanawe."

Aliendelea akidai kuwa akiwa kidato cha pili ndipo alipoanza kuishi na Sebastian hadi wakati mama mkwe alipoanza fitina.

"Niliwacha shule kwa sababu ya mapenzi na sasa nahuzunika sana kwani nilitamani sana kurudi hata kama ni mke wa pili."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be