Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamu  kutoka kijiji cha Bukembe eneo bunge la kanduyi kaunti ya Bungoma amelazwa akiwa hali mahututi katika hospitali ya rufaa ya bungoma baada ya kudaiwa kunywa sumu kutokana na kukosa chakula.

Kulingana na majirani walioshuhudia walidai kuwa mwathiriwa alipatakana akiwa na sumu mkononi kabla ya tukio hilo.

Mkuu wa hospitali ya rufaa ya Bungoma, Magarina Mayama amedhibitisha kuwepo kwa jamaa huyo hospitalini huku akidokeza kuwa hali yake imesalia kuwa mbovu.

&feature=youtu.be