mumias sugar company

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi sasa amedai kuwa serikali ya jubilee ina njama ya kuuwa uchumi wa magharibi kivyovyote vile.

Akizungumza kwenye hafla ya mazishi ya katibu wa kampuni wa kusaga Sukari ya mumias aliyeuawa kinyama juma moja lililopita  bw. Ronald  lubia,yalifanyika katika shule ya msingi ya ivona kaunti ndogo ya Sabatia, mudavadi ameelekezea kidole cha lawama serikali hiyo kwani imedaiwa kuwa serikali hilo ilikuwa imetaka pesa kutoka kwa kampuni hiyo kwa kutumia katika kampeni hatua ambayo marehemu imedaiwa kudinda na hivyo kupelekea mauaji yake.

Vilevile Mudavadi ameelezea wadi wasi wake kwamba njama kama hiyo pia imelengwa katika kampuni ya sukari ya nzoia.

Hata hivyo Mudavadi ameahidi kufatilia kitendo hicho ili kuweza  kupatikana haki kwa mjane huyo.

View Comments