Steve alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Maureen kwani alikuwa anatongoza msaidizi wa nyumbani.

"Mwanadada alituma ujumbe wa kimapenzi kwa simu yangu kimakosa, akisema vile anataka tendo la mapenzi na hapo mke wangu aliona huo ujumbe kwa simu yake." Alisimulia Steve.

Baada ya hayo mke wangu alirarua manguo zote na akavunja televisheni kwa hasira na kuondoka nyumbani. Hayo yote yalitoke mnamo tarehe 17 mwezi uliopita."

"Na si tumekuwa na yeye leo asubuhi mbona anapiga simu kwa Radio Jambo? Hayo ni maneno ya kibinafsi sielewi mbona anayaanika." Alisema Maureen kabla ya kufichua kuwa mumewe na mwanadada wa nyumbani wamekuwa wakizungumza kwa miezi mitatu.

Anawadanganya ati alitumiwa ujube, yeye ndiye alikuwa anazungumza naye. Msichana wa kazi, mtu naamini na mtoto wangu analala naye? wamekuwa wakilala naye nitamuamini aje? Siwezi msamehe." Alieleza zaidi Maureen ambaye amekuwa pamoja na mumewe kwa miaka mitatu.

Wawili hao wamejaliwa na mtoto mmoja mchanga.

Bwana Steve naye aliposkia sauti kali ya mkewe alitoweka.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be