Maafisa wa polisi katika kaunti ndogo ya Bungoma kaskazini wanamtafuta kijana mmoja kwa jina anayedaiwa kumuua kwa kumdunga kisu Martine Wafula  wakizozania msichana.

Naibu wa chifu wa Misanga Gladys Wanjala amethibitisha kisa hicho, na kuahidi kushirikiana na polisi kuhakikisha  mshukiwa ambaye kwa sasa amekwepa anakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Ameonya vijana dhidi ya kuhudhuria disco za matanga, na pia wanasiasa kuendesha kampeini nyakati za usiku kuwa watakabiliwa vikali iwapo watapatikana.

View Comments