patanisho.fresh

Kalameni mmoja amehamua kujitoa maisha kwa kujitia kitanzi baada ya kumpachika dadake wa kambo mimba katika kijiji cha Minyenya, kata ya Kamwango Kaskazini katika kaunti ndogo ya Rongo.

Kennedy Odhiambo wa miaka 21 ambaye anafanya kazi za sulubu katika mashamba ya miwa katika kijiji chao alihasi kuoa na kuanza mapenzi na dadake huyo ambaye ni mwanafunzi wa miaka 12 na wa darasa la tano.

Odhiambo alikatazwa na wazee kuhusu mapenzi hayo pamoja na tabia ya kuwamezea mate watoto wa shule.

Kulingana na chifu wa eneo hilo, Okech Boi familia yake ilikataa kumchukulia hatua za kisheria ikitaka kusuluhisha kifamilia kabla ya maji kuzidi unga.

Boi alisema babake msichana huyo Joel Omare ambaye ni ndugu wa toka nitoke wa babake mwenda zake alikwenda kwa mwenda zake na kuharibu mali za nyumbani huku akiapa kuchoma Nyumba yake.

Mkuu wa polisi katika eneo la Rongo, Jonathan Kisaka alisema kalameni huyu alionelea kujitia kitanzi kuhepa aibu kwa kitendo chake.

Kisaka ameomba Wakenya kutojihusisha kimapenzi na watu wa karibu wa kifamilia akisema huo ni utovu wa kimila.

Mwiili wa mwenda zake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Rosewood mjini Rongo ukingoja upasuaji wa kimaabara na uchunguzi zaidi.

-Manuel Odeny

View Comments