Bi Mary alituma ujumbe akiomba apatanishwe na Eric akidai kuwa wawili hao waligombana mpaka mumewe akamfukuza kwao nyumbani.

"Sahizi yamepita majuma mawili baada ya sisi kuzozana mambo ya fedha za kupeleka mtoto kusukwa. Alinieleza ningoje atanipa fedha lakini nikamngoja na hatimaye nikaamua kutumia fedha zangu.

Sasa siku nyingine nikamuomba fedha na akadai kuwa nisiwe namuitisha fedha ovyo kwani yeye sio benki huku akidai kuwa napenda fedha sana.

Hapo alinieleza kuwa kama nahisi hanishughulikii niende kwetu." Alieleza Mary ambaye bado hajaondoka kwa nyumba akidai kuwa anahisi mapenzi yameisha kwa nyumba.

"Ndoa ni nzuri nivile saa zingine chakula kina kitunguu saa zingine hakina. Shida ni eti mke wangu hana subra hakuna mambo mengi. Shida nikuwa hutaka kila kitu kipya ambacho kinatokea kwa soko lakini labda anapata sina zile fedha." Alijitetea bwana Eric kabla ya Mary kudai kuwa hata kama bwanake humpa fedha huja na mazozano mengi.

Saa zingine mke ana madharau anataka kupigana nami ananitusi nikama huniona kama duster kwa mlango. Gidi kama misamaha yake yaweza pangwa kwa mifuko yaweza jaza meli." Aliongeza Eric.

View Comments