Mamabo ya siasa imeleta tumbo joto katika ndoa, hasa ikiwa mke na mme wako mrengo tofauti.

Mwanadada Night, wa miaka 26, aliomba kupatanishwa na bwanake ambaye hajapatana naye kutoka mwezi wa Agosti 8, na anashangaa ni kwa nini.

Ikiwa imesalia saa mbili na nusu hapa Radio Jambo, kipindi kama kawaida ni GidinaGhostAsubuhi na kama ilivyodesturi mwana radio jambo Gidi huwa anaingia kitengo cha patanisho.

Wapendwa wawili hao hawakukosana kulingana na bi Night.

Alisema kwamba anahofia bwanake ana mpango wa kando, ndo maana hajishugulishi na bibi yake.

Mwanadada night alisema alikosana na bwanake tangu Agosti, ingawa wote wako mrengo wa NASA. 'Bwanangu alikuja nyumbani election na akarudi Kakamega na tangu hiyo hatujaongea, ananiambia atakuja, lakini mimi sitaki'.

'Mimi niko nairobi and amekataa kurudi nyumbani. nikimpigia simu anansema atarusi, nikimwambia anitumie fare niende kwake anakataa'.

'Tuko na miaka nne katika ndoa na tuna watoto watatu huku nairobi. ningetake kujua mahali yuko ama amepata mke mwingine, niende zangu'.

'Hataki nijuwe kwenye anafanya kazi, na saa zingine simu yake inakuwa off'.

'Gidi ningetaka unisaidie'.

Bwanake Daniel aliweza kuongea na Gidi kuhusu hili swala, na kudai kuwa mapato yake yame punguza na itabidi bibi yake aelewe, na atashugulikia baadaye. Pia alikubali alikuwa na mipango ya kando, lakini amewacha hiyo tabia.

Lakini Bi Night anaona hayo yote ni uwongo kwasababu anajua mapato ya bwanake, na labda hataki mahusiano naye. Alimgombanisha bwanake, hadi akakata simu.

Skiza Kanda ifuatayo