Mark kutoka eneo la Limuru alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Esther ambaye walikosana kwa ajili ya Sportpesa

"Tulikosana naye mwezi wa tisa tarehe mbili. Nilimuomba shilingi mia mbili ili niwekeze na nikamwambia nitamrudishia, sasa nikashinda elfu sita. Na sasa juu hakuwa na simu nikamnunulia simu ya elfu mbili na nikamwambia kuwa elfu nne zilizobaki nitatumia kama mahitaji ya nyumba.

Sasa alipandwa na mori na akaangusha chini ikapasuka. Hapo nikaondoka nikaelekea kujiburudisha na nikamnunulia nyama nusu kilo. Mke wangu alichukua ile nyama na akaitupa. Nilishikwa na hasira na nikampiga kofi moja na akavuja damu." Alijieleza Mark akidai kuwa mke wake aliondoka hadi Garissa huku yeye akiwa Migori.

Wawili hao wameoana kwa mda wa mwaka mmoja na wanatarajia kujaliwa mtoto wao wa kwanza.

"Huyo jamaa anaitwa Mark nilikuwa naskiza Radio Jambo. Naitwa Wyclife na huyo jamaa anayedai Esther ni mke wake, alikuwa mpenzi wangu nikiwa shuleni.

Nikampa mimba na huyo jamaa alikuwa amemchukua kwa miezi misaba na walipokosana Esther alinipigia simu akadai kuwa anadai kuishi nami. Sasa sikutaka kujua kama alikuwa ameolewa na pamoja tuna mtoto wa miaka mitatu." Alijieleza Wycliffe mpenzi wake Esther.

Alipozungumza nasi, Esther alidai kuwa wamesumbuana sana na Mark na hana fikra za kurudiana naye kamwe.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be