Purity Mueni alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bwanake bwana Njuguna ambaye walikosana mwaka huu mwezi wa pili.

"Tulikosania tu mahitaji ya nyumba, alikuwa anashughulika lakini hakuwa ananunua vitu ambavyo vyatosha kwa nyumba na hakuwa anataka kuambiwa. Isitoshe mamake alikuwa na wivu kila mara bwanangu anaponifanyia kitu kwa mfano nikisongwa nywele mamake anauliza mbona napoteza fedha ambazo tungetumia kufanya mambo mengine.

Mimi ni mkamba na nilipokuja Nairobi nikaskia fununu kuwa mamake alikuwa anadai kuwa nimechukulia mwanawe kamuti na kuwa mimi ni wa Illuminati." Alijieleza Mueni aliye na miaka 23.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wamejaliwa na mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu bwana Njuguna aliangua kicheko aliposkia sababu ya kupigiwa simu.

"Unajua niaje, mimi siwezi zungumza naye kwani furaha yangu ilikuwa kuzungumza na nyinyi wala staki kupatanishwe naye. Unajua alipotoka nyumbani ilibidi nimeoa, venye tu aliondoka alituma ujumbe akitusi wazazi wangu na mzee hawezi kubali maneno yake hata nipende kurudiana naye." Alijieleza Njuguna akifichua kuwa hawana mtoto kwani alimuoa na mtoto yule.

&feature=youtu.be