Nicholas alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Maureen.

"Mimi nilifanya makosa ya kwenda nje ya ndoa na kupatikana na mke wa wenyewe. Ile kitu ilifanya nifanye yale mke wangu hatukuwa tunaelewana kwani alikuwa anadai amechoka.

Isitoshe, alielekea college akiwa kwangu na wakati wa kufuzu ulipofika hakunieleza, alichukua wazazi wake na kuelekea bila kuniarifu. Hapo nilipata hasira na nikaenda nje ya ndoa." Alijieleza Nicholas.

Wawili hao wameishi kwa ndoa ya miaka 17 na wamejaliwa na watoto watatu.

Alipopigiwa simu bi Maureen alijitetea akisema, "Hana nafasi ya kumsamehe kwani alimkosea kabisa. Kama anajua kukasirika atakasirikia mwingine kwa hivyo wacha nipambane na maisha yangu nishughulikie watoto wengi."

&feature=youtu.be