Odede kutoka Nakuru aliomba apatanishwe na mama mkwe mama Salome, akidai wawili hao walikosana vibaya sana, miaka miwili iliyopita.

"Nilikuwa nimeoa na tukakosana na mke wangu kwa mambo ya nyumba na mke wangu huwa na hasira mbaya. Sasa aliondoka na kuniachia mtoto mchanga sana.

Hapo nikaamua kumshtaki kwa polisi na akawekwa ndani.

Hapo tukaanza kujibizana na mama mkwe kuhusu yale lakini hata baada ya bibi yangu kuachiliwa, bado hatujazungumza na mama mkwe. Tulirudiana na mke wangu na kusuluhisha yale maneno na tunaishi pamoja." Alijieleza bwana Odede.

Hata hivyo mama mkwe alishangazwa sana na yale mambo kwani yeye pia hakuwa na habari mahala mtoto wake alipo.

Pata uhondo kamili.

Pata habari zaidi kama hizi

&feature=youtu.be