15 December 2017 1 Min Read
Kizaaza Baada Ya Wafanyikazi Wa Bodi Ya Kuajiri Wafanyikazi Bungoma Kutimuliwa Ofisini
by Brian Ndungu Habari
Hali ya wasiwasi imewazingira wafanyikazi wa bodi ya kuajiri wafanyikazi wa kaunti ya Bungoma waliotimuliwa ofisini na bunge la kaunti hio wiki iliyopita.
Hii ni baada ya vijana wasiojulikana kuwatimua ofisini na kufunga ofisi zao na kafuli na nyororo.
Haya yanajiri baada ya wafanyikazi hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Gideon Sirai kuwasilisha kesi, yakupinga kufutwa kwao katika makahama inayoshugulikia kesi ya wafanyikazi katika kaunti ya kisumu.
Koti hio iliamurishwa kusitishwa mapendekezo ya bunge hilo la kuwatimua bodi hio ya watu sita.
-Brian Ojamaa