Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Mwibale eneo bunge la Kanduyi kaunti ya Bungoma hii leo amefikishwa katika mahakama ya Bungoma kwa kosa la kumbaka bintiye wa kambo wa umri wa miaka kumi na nne.

Vincent Walucho alikana mashtaka hayo mbele ya hakimu John Kingori na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu mia tatu au pesa taslimu alfu mia mbili.

Inadaiwa Walucho alimbaka mtoto huyo ambaye ni wa bibiye wa pili nyumbani kwake mwezi wa Oktoba mwaka jana baada ya kumdanganya na pesa na zawadi.

Kesi hio itasikizwa tatreje 2i mwezi ujao.

-Brian Ojamaa

View Comments