Lucas kutoka Thika alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye walikosana juzi.

kilichotokea nilichelewa kazini na ilinibidi nilale mle kazini kwani nafanya kazi ya taxi.

Kawaida huwa namaliza kazi mida ya saa mbili na juzi ilinibidi niendelee. Sasa kurudi nyumbani mke wangu alinuna akidhani kuwa nina uhusiano, hapo akakasirika na akaondoka na kuniachia mtoto. Alieleza Lucas.

Wawili hao wameishi kwa ndoa kwa miaka mitano.

Alipopigiwa simu bi Sarah alidai kuwa yuko kwa mamake mzazi.

"Sasa sijui bwanangu aliko lala. Sasa sijui kama alipata puncture ama alipata sponsor." Alisema.

Mimi hata nashindwa kwani hatujawahi kosania mambo kama hayo na nilipompigia simu hakushika na hapo nikashuku kuwa ana uhusiano. Sasa nilikuwa nataka kujua chenye angefanya kama angeniwacha ningejua kuwa hanipendi." Aliongeza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be