Mtangazaji Annota Raey alizindua mjadala ambao ulikuwa unawapa wanajambo fursa ya kuzungumzia masaibu ambayo wamepitia mikonono mwa wazazi wao ambayo yamewatenganisha kabisa.

Wanadada wawili walizungumza hewani na mmoja aliwashtua wengi aliposimulia jinsi babake alivyo mkata mkono mmoja kwa hasira baada yake kurudi nyumbani akiwa amechelewa.

Mwanadada mwingine naye alieleza kuwa mamake alimchoma kwa kijiko kimoto mapajani na jambo hilo bado huwa ameliweka moyoni, huku akiongeza kuwa hajazungumza na mamake mzazi kwa miaka kumi na mitano.

Soma usimulizi kamili.

Mimi nilikosewa na baba kwani alinikata mkono na panga. Nilirudi nyumbani nikiwa nimechelewa na nilipofika sikujua mpango wake, sasa alinipiga vibaya kisha akanikata mkono mmoja na sahii nina mkono mmoja. Sijazungumza naye kwa miaka miwili sasa. Alisimulia.

Saa hii ni kama miaka kumi kabla tuzungumze naye. Alinituma dukani nikapoteza 50 bob, amini usiamini aliweka kijoko kwa moto akanichoma kwa mapaja.

Sasa hiyo alama iko mpaka sahii nikienda kujifungua madaktari huniuliza nini kilifanyika. Sasa hilo jambo ndio hunitia machungu moyoni mpaka leo hadi huwa sitaki kumpigia simu.

Alipoulizwa chenye anaweza fanya akaskia kuwa ameaga dunia alidai kuwa hawezi muona akiwa uhai bali atasafiri kumzika.

Nitaenda tu kumzika kwani niki imagine roho yangu huwa mzito, isitoshe watoto wangu hawamjui. Aliongeza.

Skiza kanda ifuatayo..

&feature=youtu.be