Bwana Mwaniki alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe baada ya kumkosea sana.

Akijitetea Mwaniki alidai, "Kuna wakati nilikuwa nimeenda kazi kisumu na usiku mmoja nikampigia simu na mwanamke mwingine ndiye alijibu, kumuuliza mke wangu yuko wapi yule mwanadada akadai amepigiwa simu na mwanaume mwingine na akaondoka. Kumpigia simu ile ingine hakushika na nikapandwa na hasira na kumuandikia ujumbe mbaya nikimuambia kama ameenda umalaya basi aende alale na babake.

Sasa siku tuliyozungumza akadai kuwa hiyo siku hakuwa amefunga kazi na alikuwa ametuma jamaa fulani ndio maana hakujibu simu zangu." Alisema.

Alipopigiwa simu mkewe alidai kuwa wawili hao wameishi wakigombana tangia mwaka wa 2013.

"Alinidanganya kuwa hakuwa ameoa lakini niligundua kuwa ameoa na ana watoto wanne na huyo mke anatambulika kwo nyumbani. Licha ya hayo yote bado alikana. Ya pili nikimpa fedha hudai zimepotea kwa benki eti hajui kwenye zilienda. kwenda kwa bank alikuwa na zaidi ya elfu sitini na hakulipia mtoto karo.

Dadangu alikuwa mgonjwa alikuwa amelazwa hospitalini na wakati mamangu alikuja kunitembelea huyu jamaa akanitusi mbele yao akidai aliniokota kama chokora. Hapo niliondoka kwani hana heshima hata kidogo.

Isitoshe alitumia dadangu ujumbe akidai mimi natembea na bwanake na kuwa nina virusi vya ukimwi.

Hiyo ni ngumu kumsamehe sijawahi mweleza babangu lakini nitamweleza na chenye babangu ataamua ni chake. " Alijieleza mama Peter.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be