Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Bilibili kata ya Mukuyuni eneo bunge la Tongareni baada ya mwanamume mmoja kwa jina Mike Wanyonyi mwenye umri wa miaka 42 kuuawa na majambazi usiku wa kuamkia hii leo.

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo wakiongozwa na mwalimu Meshack Ingabo, wamesema kuwa majambazi hao waliingia mwendo wa saa saba usiku na kuhangaisha jamii hiyo kabla ya kumuuwa bwana Wanyonyi kwa kumpiga risasi tatu na kisha kumnajisi bibiye na kumlazimisha kutoa pesa.

Mwakilishi wadi ya Milima Elvis Waswa ameingilia kati na kumtaka OCPD wa Bungoma kaskazini Stephen Mwoni kuingilia na kuwanasa wahalifu hao.

-Brian Ojamaa

View Comments