Brian aliomba apatanishwe na mkewe Akinyi akidai wawili hao walikosana wiki moja iliyopita.

Kiini cha kukosana na mke wangu ni kufuli ya kufunga mlango.

Hii kufuli ni kuwa hatukuwa tunafunga mlango na nikaomba tajiri wangu kufuli na kurudi kwa boma sikuipata na kumuuliza alisema watoto ndio walikuwa nayo na hapo akakasirika na kuondoka nyumbani.

Bibi yangu alienda kwa polisi nikakamatwa na nikalala jela kwani mama ndio alichochea kuwa nilikuwa namtafuta na kisu, jambo ambalo mke wangu alidhibitisha.

Nilipoachiliwa tena nikaskia kuwa anaenda kazi Mombasa na kwa kusema ukweli sijui aliko sasa hivi. Alisimulia Brian ambaye pamoja wamejaliwa na watoto wawili.

Alipopigiwa simu bi Akinyi alidai kuwa Brayo alitoa vitu zake na watoto nje, akafunga mlango na nyororo na akachoma nguo zake.

Alidai kuwa alificha kufuli kwani mumewe alikuwa na tabia ya kufunga nyumba hadi jikoni ili asiingie. Isitoshe, alimkimbiza na panga ili amkatekate.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka mitano.

"Kurudi kwao sijafikiria kwani nimechoshwa na matusi yake kwani hata alikuwa na tabia ya kuleta bibi kwa nyumba. Amenikarisha na kuvumilia ya kutosha, wacha akae na yule anataka mimi sirudi kwao." Alizungumza Akinyi.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be