Eunice, aliomba apatanishwe na mumewe Amos akidai alimkosea sana baada ya kuiba fedha zake kupitia M-pesa.

Mimi na mume wangu tuna share pin number na kuna deni fulani nilikuwa nayo na sikutaka kumwambia. Sasa vile alienda kuoga nikachukua simu nikatuma mia tano kwa simu yangu.

Jana aliniuliza nikakataa na hapo jana alipigia watu wa Safaricom na wakampea uhondo wote." Alieleza Eunice.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa miaka miwili na Eunice anasisitiza kuwa bwanake bado amemkasirikia tangia jana.

Alipopigiwa simu bwana Amos alidhibitisha kisa hicho akidai mkewe alimuambia ana deni naye akamhakikishia kuwa atamsaidia kulipa deni lakini Eunice akachukua sheria mikononi mwake na kuamua kujisambazia hela.

"Nitamsamehe lakini hiyo sio tabia nzuri." Alieleza Amos.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be