Mwanadada mmoja kutoka Thika aliwacha wasikilizaji wengi kwa huzuni alipopiga simu katika kipindi cha 'Sema na Raey' aliposimulia jinsi anavyopitia magumu katika ndoa yake.

Kulingana na Kathrine, hajawahi pigwa katika ndoa yake ya miaka minne lakini siku ya kwanza kupitia hayo, alinyongwa na kupigwa kama mbwa kwa upanga na kuumizwa vidole.

Alisimulia kuwa kisa hicho kilitokea wakati wa maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa miaka mitatu.

Akieleza kisa hicho, alisema makosa yake makuu kulingana na bwanake ni kuwa mwanao alirudi nyumbani kutoka kwa jirani huku akiwa amebeba chakula.

Jana ilikuwa birthday ya mtoto wangu alikuwa anafikisha miaka mitatu, nami nafikisha miaka minne kwa ndoa. Alielezea Kathrine.

Sasa aki ile kichapo niliona hadi mzee wangua akanishikia hadi panga. Unaona nilipikia mtoto wangu uji na nikafua nguo na nilipomuekea chakula kwa meza mtoto akatoka akaenda kwa jirani, akarudi akiwa amebeba chakula.

Sasa nikauliza kama ni jukumu la jirani kumpikia chakula au ni langu. Aki maneno ikatoka hapo nikapigwa kama mbwa na nikanyongwa na nikashikiwa panga, alikuwa ananichapa na panga. Aliongeza mwanadada huyo huku akidai kuwa hajui la kufanya, huku akiongeza kuwa alikatwa.

 Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be