Beth Waruguru ni mama wa wasichana wawili na mke wa mume mmoja anayefahamika kama John Macharia, ni mwenye shule ya Girl Aid Foundation,shule ambayo inawasaidia wasichana kujitambua na kujijua.

Kama vile wanavyopata damu yao ya mwezi.

Pia inawasaidia wasichana kuwapa vifyaa vya wasichana kama vile wanavyo pata (menstrual period) na pia kuwazesha wawe shuleni kila wakati kutoka muhula wa kwanza hadi ule wa tatu.

"Tumechagua kusaidia wanafunzi wasichana kwa maana nambari ya wavulana iko juu kuliko ya wasichana katika mashule, lakini tukiona idadi yao iko sawa tutaweza kuingilia kati ili pia tuweze kusaidia wavulana,"

"Pia changamoto za wasichana ni mingi sana kuliko za wavulana kama vile, mwili wao ubadilika haraka kuliko wa mvulana," Alieleza Beth.

Mwalimu Alice aliweza kusema kuwa kama mwalimu unapofunza wanafunzi wa kike, mwalimu hupitia changamoto kama vile kununulia wasichana vifaa ambavyo wasichana wanahitaji kama vile visodo.

"Huwezi  muacha msichana aibike utatoa pesa zako ili uweze kumnunulia kisodo," Alice alisimulia.

Waruguru alisema kuwa hawapitii changamoto nyingi bali changamoto moja ambayo ni muhimu sana kwao.

Kama vile kuko ,Beth Waruguru ni mama wa wasichana wawili na ameoleka na mume mmoja anayefaamika kama John Macharia, ni mwenye shule ya Girl aid  Foundation. Pesa za kununua vifaa hivo vya wasichana hao, Beth pia aliweza kusema si pesa vya visodo pekee bali wasichana wengine hawana vazi la ndani la kuvaa na visodo.

"Hatupitii changamoto mbili wala tatu bali changamoto moja utapata hatuna pesa za kununu visodo pia wasichana wengine hawana vazi la ndani itabidi uwa nunulie ili uweze kuwafunza vile visodo hivyo vinawekwa," Waruguru alisema.

Caroline Kerubo ambaye ni msichana wa darasa la 8, aliweza kusema kuwa amesaidika kupitia usaidizi huo, kwa maana hajaacha shule kama wasichana wengine.

Beth ameweza kuwasaidia wasichana wa shule ya Therereka, na kupata ombi maalum kutoka shule tofauti na kuweza kuwasaidia wasichana wengi.

Kama vile Beth alivyosema na kuzungumza na Massawe akisema kuwa wanachangamoto yao kubwa kama kampuni ni pesa.

Aliweza kupata fursa ya kusema kama unaweza kumsaidia msichana asitoroke shule ama kuacha shule, unaweza kutuma chochote kupitia (paybill 181344).

&feature=youtu.be