nahashon mutua

Mwanaume aliye kuwa OCS na kupatikana na mauaji ya mahabusu ana hukumiwa leo,katika utawala wa jaji wa mahakama ya juu jaji Stella Mutuku,Nahashon Mutua alipatikana na hatia mwaka jana Desemba wa kumuuwa mahabusu.

Martin Koome Imanyara aliye kuwa mahabusu katika kitua cha polisi cha Ruaraka, na kujaribu kumuekelea Kevin Odhiambo mahabusu pia katika kituo hicho cha Ruaraka kwa mauajo hayo.

Koome alikuwa mwanabiashara a kuuza Miraa katika eneo la baba dogo,Ruaraka kaunti ya Nairobi.

Alirudi nyumbani kwake akiwa amelewa alipokuwa na mgogoro na mke wake, kisha akabeba mtoto wao wa miezi mitatu akimtishia kuruka na yeye kutoka kwa ghorofa ya nyumba yao.

Ilimbidi mke wake kupiga nduru ili apate usaidizi ambaye aliweza kuwapigia polisi simu.

Polisi waliwasili katika eneo hilo na kumkamata Koome kisha kumpeleka katika kituo cha polisi cha Ruaraka,alipofikishwa katika kituo hicho koome alikataa kuingia katika kiini cha polisi huku akidai kuwa hajafanya kitu chochote kilicho kusudia kushikwa kwake.

Ilikuwa wakati huo ambapo OCS Nahashon aliweza kuingililia ndani na kumchapa Koome na kufa papo hapo.

Polisi huyo alitumia chuma bomba kumtandika Koome, akimuacha na majeraha. Kikundi cha haki(International Justice Mission) waliweza kuchukua jambo hilo kwa uzito na kupeleka kisa hicho katika (Independent Policing Oversight Authority) na kuwapa ushahidi huo ambao uliweza kumueka ndani polisi huo.

Mshukiwa huyo alisema kuwa Koome hakuwa ana watii polisi na kisha kuenda kwa undani kuwapa wachunguzi hongo licha ya kumuekelea mahabusu Odhiambo.

"Baada ya mauaji hayo mshukiwa aliweza kujilinda kwa kumuekeleana kumtishia mahabusu PW5,"kartasi za mahakama zilisema.

Odhiambo alikuwa mwizi na kisha kutiwa baroni kwa kufanya vurugu,baadaye aliweza kuwachiliwa huru baada ya mwendesha mashtaka kupata polishi huyo na hatia.

Kesi hiyo iko katika mstari wa kwanza, kwa polisi kumuuwa mahabusu kinyume cha sheria.

Adhabu itakayotolewa na mahakama leo inatarajiwa kuwa kali mno na kuwa mfano kote nchini kwa polisi ambao wanatabia hiyo ya kuwauwa mahabusu kisha kuwaekelea wenzao.

View Comments