- Kalonzo Musyoka
- Alfred-Mutua

Aliyekuwa naibu wa rais Kalonzo Musyoka hana nyenzo za urais kwa sababu hana msimamo mmoja alisema gavana wa Machakos Alfred Mutua.

Mutua alisema kuwa kamanda mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Kenya anapaswa kuwa kiongozi ambaye ana msimamo imara.

"Huwezi ambia vikosi vya ulinzi waweze kupiga risasi, kisha uende kwa utawala wako uwaambie wasipige risasi wakati risasi enyewe ishaapigwa," Mutua alisema Jumapili.

Aliongea maneneo hayo akiwa anahotubia vyombo vya habari. Inasemekana kuwa Kalonzo ameunga mkono wito wa kura za maoni ili kuongeza kikomo kirefu cha rais Uhuru.

Kiongozi huyo wa chama cha Wiper alikataa madai hayo na kusema kuwa hakueleweka.

"Nikisema kitu huwa na maanisha, niliposema kuwa nime msamehe ndugu yangu Uhuru nilikuwa nmemsamehe na wala sikusema kuwa Uhuru ana paswa kupewa muhula wa tatu," Alieleza Kalonzo.

Wanasiasa walisema kuwa kura ya maoni ina mizizi katika kiti cha urais kwa maana inataka kuleta tena nafasi ya waziri wakuu na manaibu wake (prime ministers and deputies).

Wengine hawataki rais kustaafu kwa maana muhula wake unaisha mwaka wa 2022. Badala yake wanataka katiba kubadilishwa ili kutoa muhula wa urais.

Hata hivyo Mutua alisema kuwa yeye ni miongoni mwa waliounga mkono katiba kubadilishwa na kuanzisha tena kuwa kwa waziri mkuu na manaibu wake, lakini hajaunga mkono kutolewa kwa kikomo cha muhula wa rais na magavana.

"Hatutaki tena kurudi kwa maisha ya udikteta," Alisema Mutua.

Alibainisha kuwa wananchi wamelipa bei ya mwisho ili kutoa udikteta kupitia chama ambacho kimekuwa katika nafasi wakati wa serikali ya Kanu.

Alisema kuwa 'ugonjwa' wa viongozi wa Afrika kushikilia mamlaka umefanya kuwa maskini katika bara na Kenya haipaswi kupitia katika njia hiyo.

"Inawanyima vijana nafasi ya kuongoza nchi," Alizungumza Mutua.

Gavana huyo alisema kuwa kwa maana Kalonzo ameonyesha hana haja na kiti cha urais 2022, badala yake anapaswa kumuunga mkono kuwania kiti hicho.

"Sasa mimi ndiye kiongozi pekee wa kutoka kanda ya mashariki ambaye ametangaza nia ya kiti cha urais, mkoa unapaswa kuniunga mkono," Mutua alieleza.

Gavana huyo wa Machakos amewaunga mkono gavana wa kitui Charity Ngilu na gavana wa Makueni Kivutha Kibwana kumpiga vita Kalonzo.

Walisema kuwa hawana lolote la kuficha na hawana shida na kila mmoja wao. Jumapili Mutua alisema "Hatuna shida na Kalonzo ilhali tuna shida na siasa za umaskini," Alizungumza Mutua.

Magavana hao watatu walimlaumu Kalonzo kwa umaskini wa mgoa wa Ukambani kwa faida yake menyewe.

"Ni rahisi sana kuongoza maskini kuliko tajiri, nahakikisha kuwa wananchi wa Ukambani ni tajiri,"Alisema Mutua Jumapili.

Katika vita hivyo vya magavana hao na Kalonzo kweli zitaweza kuwasaidia wananchi wa ukambani ama zitawatawanya wananchi hao?

View Comments