- Catherine kamau
- Cate actress

Catherine Kamau almaarufu Kate Actress alisema kuwa ombi la mtoto wake kuja kuishi na yeye katika nyumba yake ndogo ndio ilimfanya atie bidii katika kazi yake.

Katika mahojiano mama wa mtindo mpya alisema kuwa mama yake mzazi aliweza kumsaidia sana kwa kumlea mvulana wake, baada ya kutoka kuishi na mama yake.

Cate kwa sasa ameolewa na Phil Karanja ambao walianza kuigiza pamoja katika kipindi cha Mother-in-law kilichokuwa katika runinga ya Citizen.

"Alikuwa mwelekezi wangu katika kipindi hicho na aliweza nisaidia kukuza kazi yangu, nampenda kwa maana ni mtu mwenye uwezo mwingi," Aliongea Kate.

Alisema kuwa majibu ambayo anapata mabaya ni akiweka picha yake na mume wake Phil, huku akisema kuwa maisha yake yamekuwa safari na mambo amepitia kisha watu kuandika mambo mabaya kumuhusu.

"Huwa nasikia vibaya watu wakiandika mambo mabaya kuhusu mume wangu na mimi, nikijua maisha yangu yamekuwa ni safari isiyo rahisi,

"Na mambo mengine pia ambayo yanahusiana na mtoto wangu huwa nasikia vibaya sana wakiandika mambo ambayo yanahusu familia yangu," Catherine alizungumza

View Comments