mambombotelarjartwork

Leonard Mambo alikuwa mtangazaji ambaye alianza kutangaza 1964.

Akiwa katika kitengo cha ilikuwaje na mtangazaji Massawe Japanni alisema kuwa alipenda kazi ya utangazaji akiwa shule ya upili.

"Nilikuwa nangoja wanafunzi wakiwa kwenye mabweni wanasoma na chukua gazetti kisha naanza kusoma habari, wengi waliweza kunikemea na kusema kuwa nawapigia kelele kwa maana wanasoma,

"Siku moja niliweza kusoma habari nikiwa bado shuleni na mmoja wa wanafunzi akaniambia vile ananiona na weza kuwa mtangazaji," Alieleza Mambo.

Mbotela alilelewa mjini Mombasa na katika kazi yake ya usanii anaitwa Ibrahim Juma. Aliweza kusema kuwa huwa anaitwa katika maharusi kama mfawithi na pia kwenye klabu kuimba.

Ndoto yake ya utangazaji iliweza kupingwa na mwendazake baba yake, ambapo alikuwa anasema kuwa kazi hiyo si nzuri.

"Baba yangu aliweza kukataa niwe mtangazaji lakini niliweza kupenda sana utangazaji mwaka wa 1964 niliweza anza utangazi rasmi niliweza kuandikwa na mwendazake Stephen,

"Niliandikwa kama (programme Assistant )katika runinga ya KBC iliokuwa inaitwa VOK wakati huo," Leonard alizungumza.

Leonard ameweza kuuwawa sana katika mitandao na kisha hakuwa anajua watu wanampigia simu kumuuliza kama yuko sawa.

"Kuna siku niliweza kupigiwa simu na watu zaidi ya elfu wakiniuliza ama ni mimi na nimefufuka lini ilhali nimeweza kufa katika mitandao ya kijamii,

"Niliweza kung'ang'ana na kisa hicho na ninawaimiza serikali iweze kuweka kanuni katika mitandao ili wasiweze kuwauwa watu kiholelaholela," Alisema Leonard.

Katika kipindi cha JEE HUU NI UUNGWANA alianzisha mwaka wa 1966 miaka miwili baada ya kuandikwa katika stesheni ya VOK.

"Tulikuwa tumeenda mkutano katika hoteli ya kifahari ya PanAfric na kisha watu kadhaa wakachelewa na pia kuhudumiwa kukachelewa,

"Wenzangu waliweza kupiga simu huku na huku wakiwaarakisha wenzetu na pia waliweza kumharakisha muhudumu ambaye alikuwa anatuhudumia,

"Niliweza kuwaonya nikiwaambiwa kuwa subira huvuta heri na hapo ni hotelini si nyumbani, sasa hapo ndipo niliweza kuwa na wazo kama hilo la kuanzisha kipindi kama hicho," Alisema Mbotela.

Hakuweza kuandika hati (script) ya kipindi hicho bali aliweza kusema kuwa ilikuwa talanta kutoka kwa mungu.

"Sikuandika hati ya kipindi hicho kwa maana naamini kuwa ni talanta kutoka kwa Mungu," Mambo alisema.

Ni kipindi ambacho kilimuezesha kujulikana kwa sana nchini na pia kujulikana na marais wa Kenya kwa kazi yake nzuri ya kipindi hicho ambacho kilikuwa kinaonyesha katika runinga ya KBC.

Mtangazaji huyo ana mke mmoja na watoto watatu ambao ni wanabiashara bali hawakufuata nyayo za babayake.

"Sina mtoto ambaye amenifuata bali nina mpwa ambaye ni mtangazaji wa mpira," Alieleza Mambo.

Aliweza kustaafu 1997, bali kwa ajili ya kipindi chake cha je huu ni uungwana aliweza kuambiwa aendelee na kipindi hicho katika runinga ya KBC.

Katika mwaka wa 1984 Leonard aliweza kuitwa ili aweze kufanyia rais mstaafu Moi kazi na kuweza kufanya chini ya rais huyo.

View Comments