1897949(2)

Ni kifo ambacho kilimkumba wakili Robert Chesang Jumapili akiwa nyumbani kwake, aliweza kuishi katika hoteli kwa zaidi ya miezi mitatu, na kutumia shillingi 500,000.

Kati ya mwezi wa Septemba 19 na Novemba 11 alitumia shillingi 446,250 katika hoteli ya sandalwood baada ya kuzuiliwa kwake nyumbani.

Marehemu aliweza kurudi nyumbani kwake Moke Gardens, Lukenya kaunti ya machakos wiki kadhaa zilizopita kabla ya kupatana na kifo chake cha unyama.

Aliweza kupata nafasi tu ya kuwa katika nyumba yake baada ya mke wake Maisy Omungala ambaye ni hakimu alipoenda kufanya kazi maeneo ya Nyeri Disemba mwaka jana.

Katika kesi namba 47 ambayo iliweza kuwakilishwa mahakamani kwa ajili ya wakili huyo kuwa na vurugu na kumtesa mke wake, inadaiwa kuwa Chesang alilazimishwa kutoka nyumbani kwake, kwa maana mke wake alikuwa mwenye vurugu na pia aliwatumia polisi kumnyanyasa na kumtisha.

Wakili Chesang aliweza kuomba mahakama kumpa ruhusa ili aweze kuishi nyumbani kwake bila masharti yeyote, alisema kuwa vifuli vya nyumba yake viliweza kubadilisha na pia nyumba hiyo ilikuwa chini ya ulinzi wa polisi.

Aliongezea na kusema kuwa Maisy aliweza kuwahamisha watoto wake shule na kumkataza pia kuwaona watoto hao.

"Kutoka Agosti mpaka sasa hivi nmepoteza mali yangu ambayo nimetafuta tangu nilipoanza maisha yangu ya ndoa, kwa sababu ya vitendo haramu vya washiriki." alisema Chesang katika kiapo.

Aliweza pia kuuliza mahakama kumkubali atumie gari zake za lexus na premio, ambazo zilidaiwa kuwa zinatumiwa na polisi.

"Naomba kuwa mahakama iweze kuwaambia polisi na maafisa wengine wa mahakama waache kutumiwa na mke wangu kuninyanyasa na kunitisha, na waache kutumia gari zangu kama mali ya uma," Chesang aliwakilisha.

Kesi yake iliweza kuhamishwa mara tano baada ya hukumu kufanyika.

Septemba, 24, mwaka jana aliweza kumpigia simu hakimu mkuu Linus Kassan na kuzungumza kuhusu kesi yake ambayo ilikuwa mahakamani.

"Mimi ndiye mwenye usukani katika mahakama ya Mavoko na nimemwambia hakimu aweze kuhairisha utawala wa kesi ambao ungefanyika Ijumaa 21 kuhusu mgogoro huo wa nyumbani,

"Nitahakikisha kuwa hakuna hukumu yoyote ambayo itatolewa kuhusu jambo hilo hakimu haendeshi kesi vile ninavyotaka," Alisema hakimu.

Katika majibu kupitia ujumbe wa simu, hakimu huyo alisema kuwa hajawahi ingililia kesi ya wakili Chesang, wiki hiyo hiyo Kassan aliweza kuhamishwa na kupelekwa katika mahakama ya kaunti ya Machakos.

View Comments