rachelmwiziwamabavu

Rahab Nyawira alikuwa mwizi wa mabavu kisha akakuja kushikwa na kufungwa kwa miaka sita, alisimulia hadithi yake katika kipindi ukipendao cha ilikuaje.

Alifungwa kwa kuiba magari na wenzake wanne. Rahab hakuzaliwa akiwa mwizi bali aliweza kufunzwa na rafiki yake wa kutoka utotoni.

"Nilihusishwa na rafiki yangu katika wizi, nilianza kuiba kama mtu wa mikono yaani nilikuwa napewa kadi naenda kutoa pesa,

"Kisha mwenye kadi hiyo ya benki tunamshika mateka, ndiposa asiweze kutupea (pin) ambayo haistahili, nilikuwa mimi peke yangu na wanaume wanne,

"Tulianza kazi hiyo tangu mwaka wa 2008 hadi tulipokamatwa mwaka wa 2012, baada ya muda usiokuwa mrefu niliweza kupandishwa cheo kisha nikaanza kufunzwa jinsi ya kufanya kazi na bunduki." Alisimulia Rahab.

Rahab alivutiwa na kazi hiyo kwa sababu mara ya kwanza waliweza kuiba shillingi 800,000, kutoka kwa watu tofauti mshahara wake wa kwanza ulikuwa zaidi ya shillingi 100,000.

"Niliona kazi hiyo inalipa mzuri kwa masaa machache, siku moja tuliweza kuiba gari kisha tukaenda kujivinjari, tuliweza kumtuma mmoja wetu pombe,

"Alienda na kuanza kuwatishia watu waliokuwa katika klabu hicho, hapo ndipo polisi waliweza kutujua na kisha tukatoroka,

"Tulienda maeneo ya namanga kisha tukaenda nchini Tanzania mafichoni." Alisema Rahab.

Walipofika maeneo hayo Rahab hakuwa na amani moyoni mwake kwa maana miongoni mwa waliokamatwa na polisi alikuwa kijana ambaye alikuwa amemfunza wizi.

Waliwasiliana kwa njia mbalimbali ndipo siku moja kijana huyo mwenye alikuwa mwanafunzi chuo kikuu cha Nairobi, aliweza kuwauza kwa polisi.

"Nilipata kijana huyo amejaribu kunipigia ndipo, niliweza kumpigia na namba ingine kisha akaniambia amachiliwa,

"Niliweza kufurahi kisha nikamwambia tupatane mahali huwa tunapatana, tulipofika hapo tulipata watu wengi wakiwa na gari zao,

"Mmoja wetu aliuliza hawa ni akina nani bali tulipuuza kisha tukasema ni matajiri, kumbe walikuwa ni polisi,

"Baada ya muda mfupi polisi hao waliweza kutuambia tujisalimishe kumbe huyo kijana alikuwa ametuuza kwa polisi," Rahab alisema.

Wakati huo Rahab hakuwa amefikisha miaka 30, hapo ndipo aliweza kukamatwa na kufungwa kwa miaka sita.

Nyawira alisema kuwa hakuweza kubadilika akiwa jela bali aliweza kuwa mbaya zaidi huku ikimlazimu aanze kuuza dawa za kulevya, aliweza kushtakiwa kwa wizi na vurugu.

Rahab aliweza kuachiliwa huru na kisha kuwa afisa katika shirika la (African Prison Project) na kuwasaidia wafungwa ambao wameshindwa na kesi zao.

View Comments