- James Orengo
- 1829186

Maneno ya nipe nikupe yalizidi hadi pale seneta wa Siaya James Orengo alipoapa kuwa atahakikisha kuwa naibu wa rais William Ruto ataweza kurekodi kauli yake kwa polisi kuhusu uchunguzi wa kashfa ya bwawa la Kimwarer na Arror.

Orengo alisema kuwa inakaa Ruto ana habari zaidi kwa sababu anasisitiza kuwa billioni saba ndizo zilizopotea bali si billioni 21.

"Kama rais hataweza kumfanya naibu wake kurekodi kauli yake kufafanua matamshi yake, mimi mwenyewe nitaweza kumfanya arekodi kauli na polisi." Orengo alisema.

Aliongea Jumamosi eneo la Sega wakati wa maandamano ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Ugenya, aliongeza na kusema kuwa hakuna yeyote ambaye yuko juu ya sheria.

Alisema pia kama kiongozi hataweza kukaa chini na kuangalia pesa za walipa ushuru zikiwa hazijahesabiwa.

"Ruto ndiye ameweza kualika nchi kujua ukweli hasa juu ya fedha ambazo zimepotea, juu ya mabwawa baada ya kutatanisha twakimu." Alizungumza Orengo.

Seneta huyo alimuuliza rais Uhuru Kenyatta aweze kusimama kidete katika mapigano hayo ya rushwa.

Orengo pia alimuomba Uhuru azidi kusukuma kukamatwa kwa watu binafsi ambao watapatikana na hatia licha ya maneno ya wanasiasa wengine kusema kuwa jamii zao zinalengwa.

"Rekodi ya serikali ambayo inaonyesha watu ambao wameweza kupatikana na hatia ya rushwa na ambayo iko katika mikononi mwa rais,

"Inaonyesha wakikuyu 43, waluo 18, waluhya 11 na wakalenjin 6 wameweza kupatika na na madai hayo." Orengo alinakili.

Baadhi ya viongozi wa eneo la Rift Valley waliweza kusema kuwa mkoa huo umeweza kulengwa na serikali. Orengo alisema kuwa kama kuna jamii ingekuwa na malalamishi ni jamii ya Wakikuyu.

Mbunge wa Ugunja Wandanyi aliweza kumuambia Uhuru aweze kupambana vilivyo na watu binafsi ambao watapatikana na hatia ya rushwa.

"Nimekuwa katika bunge kwa muda wa muhula miwili, nikiwa na mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi na sijawahi msikia ama kumuona akiongea neno ata moja la kiingereza juu ya rais kuhusu vita dhidi ya kashfa." Aliongea Wandanyi.

Mwenzake Elisha Odhiambo aliweza kuuliza swali kuwa. "Wakati gavana Obado na gavana Ojaamong waliweza kushikwa kwa ajili ya madai ya kashafa waluo na waluhya waliweza kumuita rais Uhuru majina." Elisha aliuliza.

Odhiambo aliweza kumwambia Sudi asifikiri kuwa jamii yake ni maalum.

View Comments