Ndege aina ya Boeng 737 Max, imepata pigo baada ya tukio la Jumapili lililohusisha ajali ya ndege ya Ethiopia, ambapo abiria 157 walipoteza maisha yao.

Ndege hiyo iliyoratibiwa kutua katika uwanja wa ndege wa JKIA ilianguka dakika sita baada ya kupaa.

Ajali hiyo ilikua ya pili yote ikihusisha aina ya ndege ya Boeng yenye usajili 737-Max.

Katika kisa cha kwanza, mwaka wa 2018 mwezi wa kumi, ndege ya kampuni ya Lion Air ilianguka kwenye bahari ya Java na kuwaua abiria wapatao 189.

Kampuni ya ndege ya Ethiopia ilisitisha safari zake za ndege inayohusisha boeng 737 max baada ya kisa cha hivi punde.

Mataifa mengine ambayo yamehairisha safari za ndege ya Boeng 737 Max ni Australia, ziwa la Singapore, Uchina, Indonesia pamoja na taifa la Thai.

Kampuni inayotengeneza aina za ndege za Boeng 737 Max imeamrishwa na shirika la Marekani kufanyia ukarabati ndege hizo haraka.

View Comments