RailaOdingaatToiMarket

Kinara wa upinzani Raila Odinga amewalaumu wanyakuzi wa ardhi na mabwenyenye katika kisa cha moto kilichozuka katika soko la Toi linalopatikana katika mtaa wa Kibra na kuharibu mamilioni ya mali.

Raila alifika katika eneo hilo kuwapa pole wenyeji kwa kupoteza mali zao. Moto huo uliripotiwa kuanza usiku wa manane Jumanne ya tarehe 12 na kuenea kwa kasi.

“Hii sio mara ya kwanza moto kuzuka Toi. Inaonekana imechomwa kimakusudi. Nina hakika wanyakuzi wa ardhi walipanga njama ya kuchoma ili kesho waje watimue wenyeji. Nawapa hakikisho kwamba hilo halitafanyika,” Matamshi ya Raila.

Aidha, Raila amesema atashirikiana na viongozi wengine kuhakikisha mikakati maalum imewekwa ili tukio hilo lisitendeke tena.

Pia amesema pana haja ya uchunguzi kuanzishwa mara moja ili kubaini chanzo cha moto huo.

Raila vile vlie amesema vita vinavyoendelea dhidi ya ufisadi havilengi jamii Fulani kama wanavyodhania wengine. Amewataka watakaopatikana na hatia kubeba msalaba wao wenyewe.

Raila aliandamana na viongozi wengine wa upinzani akiwemo mbunge wa Mathare Anthony Oluoch.

View Comments