- Kiunjuri
- thwake

Makatibu wawili wa mawaziri waliitajika katika ofisi ya Kurugenzi ya uchunguzi ya jinai (Directorate of Criminal Investigation) katika uchunguzi wa bwawa la Arror na Kimwarer unaoendelea.

Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa na waziri wa kilimo Mwangu Kiunjuri wataweza katika ofisi ya DCI iliyo katika barabara kuu ya Kiambu.

Wawili hao wali tarajiwa kuenda ofisini humo kwa masaa tofauti kwa uchunguzi huo unaoendelea.

Wawili hao walisema kuwa kama rais Uhuru amekosana na naibu wake William Ruto awache kuiwapa adhabu jamii ya Kalenjin kwa ajili ya ugomvi wao.

Uchunguzi huo uliweza kufanya DCI kumchunguza na kumuuliza maswali Rotich kuhusiana na mabwawa hayo.

Walipa ushuru walisema kuwa shillingi billioni 21 zimeweza kupotea ambazo zilikuwa zimetengwa kwa kujenga mabwawa hayo, lakini serikali iliyoongozwa na Williama Ruto na mweka hazina Henry Rotich wakisema na kusisitiza kuwa billioni 7.8 pekee zimeweza kutumika kuwa lipa wanakandarasi hao malipo ya mapema.

Rotich aliweza kuchunguzwa kwa siku nne na wachunguzi wa DCI bali mkurugenzi wa (Kerio valley Development Authority) David Kimosop akifanyiwa uchunguzi  na kuulizwa maswali kwa siku mbili pekee.

View Comments