Waziri mteule wa elimu Prof. George Magoha alisema kuwa hataki kazi yoyote kama wabunge wataingililia kazi anayofanya, aliongeza na kusema kama wambunge hao wanafikiria ameenda kufanya biashara ya nyani waweze kuweka kazi yao.

Mpasuaji, profesa na mwanabiashara Magoha alisema kuwa hajawahi shindwa na kitu chochote na hataweza kuvumilia 'Monkey business' kama atachukua usukani katika wizara hiyo.

"Katika miaka yangu yote ya upasuaji, naweza jivunia nikisema kuwa hakuna mtu yeyote ambaye alikufa akiwa katika meza ya operesheni,

"Na nikishindwa katika nafasi hii itakuwa mara ya kwanza, na sikuweza kutetea uteuzi wangu bali ni utalaamu wangu,

"Kama hilo ndilo mnataka basi nitawatolea, lakini kama kuna shughuli ambazo hazieleweki mnaweza kuweka kazi yenu." Magoha aliwaambiwa wabunge alipokuwa kwenye mkutano kwa uteuzi.

Waziri huyo alisema kuwa anapenda kufanya kazi kutoka upande wa nyuma kuenda mbele, alionyesa ujasiri wake kuwa ataweza kuleta ubora katika sekta ya elimu.

"Ninapo weka macho yangu kwa kitu fulani, kwanza ninaangalia ninachotaka kufikia, alafu kutoka hapo ninaanza kazi yangu." Alieleza Magoha.

Aliweza kujipiga kifua na kujigamba kuwa na mali ya millioni 250, na kujitambulisha kama mkristo kamilifu wa kanisa la katoleki.

Profesa huyo aliwaambia maafisa wa wizara ambao wana shuguli za rushwa waweze kabadilisha mienendo yao kabla hajawatambua, aliwaonya pia ambao wanawaomba wasichana wa shule wafanye ngono na wao huku akisistiza kuwa siku zao zimehesabiwa.

Pia aliingia katika mjadala wa mitandao ya filamu za ponografia na kupendekeza iweze kufungwa.

"Kama bunge hili itakubali uteuzi wangu, basi ombeni Mungu sana nisiweze kuwapata mkiwaambia wasichana washule wapanue miguu yao." Magoha alisema.

Aliweza kusema kuwa na uwazi na ushiriki katika elimu ya ngono. Magoha alionyesha nia yake kuweka sura katika mtaala mpya, aliitisha fedha za kutosha ili kuhakikisha mafanikio ya utekelezaji.

"Ukweli ni kuwa tuko nyuma sana katika mtaala huo mpya, Rwanda wamefanya na pia Sudan kusini wamefanya, na maanisha kuwa nchi yetu ya Kenya inapaswa kuwa ishaanza mtaala huo na kisha nchi zingine zifuatie,

"Nitaenda kuamsha mtaala mpya." Alisema Magoha.

Aliweza kuunga mkono kuongezwa kwa karo ya vyuo vikuu mpango ambao ulikuwa umeanzisha lakini si zaidi ya vile ilikuwa imeongezwa.

Alisema kuwa ni lazima karo iongezwe ili iweze kuwa sawa na nyakati hizi za kiuchumi, Magoha alihaidi wanafunzi ambao usajili wao uliweza kukataliwa kwa kutumia vyeti vya kazaliwa visivyo halali kukalia mtihani wa kitaifa.

Mwezi jana (Kenya National Examinations Council) walikataa usajili wa wanafunzi 370,000, baadaye iliweza kusema kuwa wanafunzi hao watapewa nafasi ya pili kurekebisha makosa yao na kisha kukalia mtihani.

View Comments