massawe (1)

Jamaa kwa jina Caleb Onyango ambaye ni mzaliwa wa Kisumu ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuwaje na Massawe Japanni.

Onyango alisimulia kuwa maisha yake yalibadilika baada ya mkewe kupata ajali huku akiwa na uja uzito wa miezi mitatu.

Alisimulia kuwa kwa bahati na mapenzi yake mungu, licha ya mkewe kuvunjwa mifupa, mimba ile haikuguzwa lakini sasa inambidi asalie nyumbani ili amtunze mkewe.

Alisema: Tarehe kumi na saba Januari mwaka huu, mke wangu kwa jina Catherine Wanjiru aligongwa na gari na akapata majeraha baada ya gari lile kumlalia. Wakati huo alikuwa mja mzito.

Nikipata habari nilikuwa nyumbani na ndipo nilipigiwa simu baaada ya wasamaria wema kumpeleka hospitalini.

Kimiujiza mimba yenyewe haikuguswa katika ile ajali na nadhani lile tukio lilibadilisha maisha yetu.

Sasa hivi mke wangu yupo nyumbani na anaendelea na matibabu, atafanyiwa upasuaji mtoto akiwa na miezi nane kwani daktari alisema hataweza kujifungua kivyake.

Aliongeza akisema kuwa ajali ile iliumiza mfupa wa pelvic na sasa mkewe hawezi fanya kazi na sasa hushinda amelala.

Alidai kuwa aliyesababisha ile ajali ni kama alikuwa mlevi na alikuwa anahepa kugonga gari la abiria na hapo akamgonga. Alipomgonga gari ilianguka kwa mtaro huku mkewe akiwa chini ya gari.

Kama ni kwenda msalani mimi ndiye humsaidia licha ya watu kuniambia kuwa nafaa kumtenga mke wangu.

Aliongeza.

Mimi ni mluo na kuna marafiki wangu ambao walikuwa wakiniambia kuwa nafaa kumtenga kwani yeye sio wa kabila langu.

Lakini the strength of a man is measured by the length you will go for your wife. The recent events have brought me closer to God kwani wakati mwingine najipata naomba ama marafiki zangu wananipa nguvu. 

Onyango anasema kuwa tendo hilo limemfunza kuwa maisha ni mafupi na yaweza badilika wakati wowote.

Aliongeza kuwa serikali yafaa iangazie mambo ya matibabu kwani pia wao hawakuwa wanasaidika katika zile hospitali walizotembelea.

Ukitembea hizi hospitali za umma unaeza shangaa, mimi hujiuliza mbona hawa madaktari mbona huwa wanagoma kwani hawafanyi kazi inavyofaa.
View Comments