josphat nanok

Gavana wa Turkana Josphat Nanok amewaomba wanasiasa na pia wakenya kwa jumla wanaopangia kuwasaidia wananchi wanaokumbwa na njaa, kufanya vile kwa roho safi.

Akizungumzia katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi siku ya Jumanne, Nanok aliwaomba wafadhili hao kutotangazia watu kila wanapofanya jambo njema.

Alisema: Nawaomba wakenya wanaotaka kusaidia wana Turkana wasaidie na wanyamaze. Katika mila yetu ukitaka kusaidia saidia na unyamaze na uwaachie yule mtu mungu wake sio kutangazia kila mtu. 

Akizungumzia swala la ukame ambalo limekumba kaunti yake ya Turkana, Nanok amesema kuwa hali iko katika hatua ya kutisha. Alithibitisha kuwa hali hiyo pia iimechangiwa na upungufu wa maji, jua kali na pia ukosefu wa usalama.

Mara ya mwisho kuwa na shida ya ukame ni mwaka wa 2017. Saa hizi viwango vya joto mchana ni digrii 45 huku viwango usiku vikiwa 30. 

Pia swala la usalama limechangia kwani tuna mipaka kadhaa inayozunguka Turkana na kumekuwa na vita vya jamii tofauti katika mipaka hii.

Aliongeza:

Tulikuwa tumeweka amani kwa miaka mitatu na West Pokot na watu wakaishi vyema bila shida lakini juzi ugomvi ukaanza kati ya jamii hizi mbili huku watu wakiiba mifugo.

Tulikutana na Matiang'i na tukasema suluhu ya hii ni polisi kukamata wanaofanya haya kwa sababu mazungumzo inakuwa ngumu kwani wakaazi huuliza mbona watu wanaiba mifugo na hawakamatwi?

Nanok alisema kuwa juhudi zao za kuchimba mabwawa ya maji hukumbwa na maji ya chumvi na pia sehemu kavu kavu.

Aliongeza  kuwa maji kutoka ziwa Turkana hayawezi tumika kwa utumizi wa nyumbani au ukulima kwani ya madini ambayo labda yasafishwe.

Nategea nione kama nitapata mabwawa angalau tano kati ya 31 ambazo waziri Kiunjuri alitangaza yatajengwa kote nchini.

Lakini tayari kuna sekta za kibinafasi ambazo zimeanza kuonesha nia za kushirikiana nasi ili kutuwezesha kushughulikia maswala ya maji.

View Comments