eudias
Katika kipindi cha Bustani la Massawe na Eudias Kigai, alipiga simu mwanadada kwa jina la Becky.

Mama huyu wa watoto wawili alipiga simu akiwa na lalama kuwa bwanake aliyemtaja kama Amos ametelekeza watoto wake wawili huku akimwacha mkewe akiteseka.

“Hajawahi kupiga simu wala kununua nguo za mtoto,” alisema Becky.

Mtangazaji Eudias alimpigia simu Amos ili kuweza kujua kiini cha tatizo kilichosababisha bwana huyu asishughulikie familia yake. Kipindi hiki huwa kinahusisha maswala ya ndoa hususan kuangazia wanaume ambao wamepachika wamama mimba na kutoweka.

Amos alifunguka bila kusitasita dhuluma alizozipata kutoka kwa mwanamke huyu aliyekuwa amemuoa kwa kipindi kirefu kabla ya ndoa yao kuvurugika.

Bwanake Becky alisimulia jinsi alivyodharauliwa na majirani katika ndoa hii. Alidai mwanamke huyu ni mlevi kupindukia na amewahi kuchapwa kichapo cha mbwa katika klabu akimuokoa mkewe.

Amenipea gharama kubwa sana. Anatoroka kwangu anaenda kwa bar kulewa nimemtoa kwa klabu mara nne sasa. Nishawahi kuchapwa nikimtoa kwa bar hadi pombe ikamwagika mpaka nikaambiwa nilipe shilingi elfu sita.”

Wawili hawa wamezaa mtoto ambaye ana umri mchanga wa miezi nane. Bwanake alieleza jinsi Becky alikuwa anachapisha picha za wanaume tofauti tofauti katika mtandao wa kijamii wa Facebook huku akiwaita baba wa watoto wake.

Jinsi inavyodhihiri ni kuwa Amos hamtaki tena mwanamke huyu mwenye hulka na tabia ya ulevi. Anasimulia jinsi alivyokuwa ananunuliwa bia na walevi wanaume na kuja nyumbani akiwa mlevi.

Amos analalamika jinsi mwanamke huyu anavyomgombeza bibi wa pili aliyemuoa alipomtema huku akiongeza kuwa aliwahi kumpa nasaha abadilike katika vikao na chifu na wamama wa kijiji ili arudi na kuitunza familia.

Amos amemalizia kwa kutoa kauli yake ya mwisho kuwa hangependa tena kuwa na uhusiano na mwanamke wa sampli hiyo na kumtaka afanye DNA ya mtoto iwapo atakuwa wake ampelekee “kama ni mtoto wangu aende afanye DNA na anipee mtoto na yeye aende akashike mambo yake”