- aa02
- aaa32

Mwanasiasa maarufu nchini Uganda na ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kuupinga uongozi unaodaiwa dhalimu na wa kidikteta wa Yoweri Kaguta Museveni jumatatu ya leo ametiwa nguvuni katika kitongojiduni cha Busabala nchini humo.

Maafisa wa polisi walitumia nguvu isiyo ya kawaida kuingia katika gari lake na kumtia nguvuni mapema asubuhi. Kufikia sasa hakuna taarifa zinazoonyesha aliko Bobi Wine. Waandalizi wa fiesta hii iliyopangiwa ya pasaka ni mojawapo ya watu waliokamatwa katika mchakato huu.

Waandamanaji ambao ni wafuasi wake walipata wakati mgumu waliporushiwa maji yanayowasha mwilini pamoja na gesi ya kutoa machozi katika makabiliano makali na maafisa wa polisi.

Rais wa Uganda Yoweri alikuwa awali amefutilia mbali mikutano katika  sehemu za burudani iliyosheheni siasa za kuipinga serikali. Mkali huyu alibaniwa kufanya fiesta na ambalo alikuwa ameiratibisha kuifanya ili kuwakonga nafsi mashabiki wake  inayofahamika kama One Love nchini humo.

Wine alikuwa ameita vyombo vya habari kuvihutubia kuhusu kufungiwa kwa tamasha lake na ambalo lilikuwa lifanyike msimu huu wa pasaka pindi alipokamatwa na kupelekwa kusikojulikana.

Robert Kyangulanyi  almaarufu kama bobi wine  sio mara yake ya kwanza kukamatwa. Baada ya mbunge huyu wa Kyadondo mashariki  kukamatwa ,ameonyesha ujasiri kwa wafuasi wake katika mitandao ya kijamii msanii huku akionyesha kutokata tama katika vita dhidi ya utawala katili na wa kidikteta

View Comments