- aa02
- aaaaaaaaaaaaa

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umelaani kitendo cha kumhangaisha msanii na mwanasiasa Bobi Wine kwa kumkamata kwa nguvu na kumfungia kitu na ambacho ni ukiukaji wa haki za binadamu.

’Viongozi imara huwa hawanyamazishi raia wao. Mataifa yanayokuza demokrasia huwapa wananchi uhuru wa kuongea na kuikosoa serikali”

Kitendo cha kumtia nguvuni kufikia sasa kimepata kuvutia hisia za viongozi wengi duniani huku sababu za kumfungia msanii huyu zikielezwa kama kutofuata masharti yalikuwepo ya kutofanya fiesta sikukuu iliopita ya pasaka

Kufutilia mbali tamasha zake tatu alizozipanga kunamsababishia hasara kubwa kwa kutumia hela kuyaratibisha. Hali kadhalika inakadamiza haki na uhuru wake wa kutangamana na waganda wenzake

Mwananasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi almaarufu kama Bobi Wine atasalia katika kizuizi cha nyumbani kwa muda usiojulikana.Hii ni kwa  mujibu wa taarifa iliyotolewa na  mkuu wa polisi nchini humo. Hatua hii inaaminika wameichukua ili kumzuia mbunge huyu  wa Kyadondo Mashariki kutwaa barua rasmi  katika makao makuu ya polisi na kuomba ruhusa ya maandamano ya amani .Kwa kufanya kitendo kama hiki kunatishia usalama wa taifa kwa mujibu wa vyanzo mbalimbli nchini humo.

Maswali yasiyo na majibu miongoni mwa wengi ni  kwa nini serikali ya Museveni mara kwa mara umzuia mkali huyu kufanya maonyesho pindi tu alipojitosa katika siasa. Waziri wa usalama wa ndani nchini humo ananukuliwa  kusema kuwa msanii huyu ukiuka masharti ya kazi anayoekewa.

View Comments